Kwa
kawaida mama wakwe wanachukuliwa kuwa na ubaridi hatari kama baridi ya
Mbeya. Lakini, kuna baadhi yao ni tofauti kabisa. Wapo wenye uvuguvugu
wa kimahaba na upendo usiokuwa na kifani kwa wake wa watoto zao. Wakati
huo huo kuna wanawake ambao wanadai kuwa hawana uhusiano mzuri na wakwe
zao, lakini kwa chini chini wanatamani sana kuwa na uhusiano mzuri na
mama mkwe. Kujua kama umo kwenye kitabu cha moyo wa mheshimiwa mama
mkwe, basi hizi ndizo ishara na dalili za kukuonesha hilo: 1. Anapokuulizia mara kwa mara: Baada
ya shamrashamra za harusi iliyofana vizuri, mama mkwe anatulia huku
akiwa mwenye furaha. Anakupigia simu kuuliza hali yako. Anataka kujua
lini utamtembelea. Kwa ufupi unakuwa kama mwanaye kwake na moyo wake
umejawa mahaba juu yako.
2. Anapokutembelea muda wowote: Sio
kawaida kwa mama ambaye umri wake umesonga kufunga safari ndefu kutoka
kijijini kwa ajili ya kumtembelea mwanaye pekee. Wamama wengi wazee –
isipokuwa wachache – hawapendelei kuwatembelea watoto wao kwa sababu ya
wake zao.
3. Anakutumia au anakuletea zawadi: Anapokutembelea
haji mikono mitupu. Anakuletea yule jogoo mwenye kilo 7, kiroba cha
mahindi, ndizi, kunde na chochote kizuri kutoka kijijini. Usidhani kuwa
hayo anayafanya kwa sababu ya mwanaye wa kiume. Bali ni kwa sababu wewe
mke wa mwanaye ni mke alimkubali pia.
4. Anakupigania: Mama
mkwe anayekupenda atakupigania na kukutetea kuhakikisha kuwa heshima
yako haivunjiki. Hata ukiwa na msuguano na mume wako, utaona anakuwa
upande wako na kutuliza mambo.
5. Watu wako ndio watu wake: Tangu
ulipoolewa na mwanaye, mama huyu amekuwa karibu sana na watu wako. Yuko
karibu na mama yako na shangazi zako. Hakosi shughuli za furaha na
huzuni za familia yako.
6. Anataka usaidizi wako wa jikoni: Kuna
wageni wamekuja nyumbani kwake, atakuuliza aina ya chakula ambacho
ungependelea kipikwe. Hata kama kuna wanawake wengine, bado atasisitiza
ushiriki katika upishi. Mara nyingi baadhi ya wanawake hulichukulia kwa
mtazamo mbaya jambo hili, lakini ukweli ni kwamba hiyo ni kama cheti
unachopewa na mama mkwe.
7. Anapokuzungumzia vizuri mbele ya marafiki zake : Wamama
wengine wanapolalamika kuhusu wake wa watoto zao ambao wana muonekano
mbaya, kucha za bandia, nywele za bandia na wasioweza kupika chakula cha
watu 20, mama mkwe wako yeye anakusifia tu.
8. Anajawa na wasiwasi unapokaa kwa wazazi wako muda mwingi kupitia kiasi: Unapowatembelea
ndugu zako na ukakaa huko kwa zaidi ya siku moja, mama huyo hukosa
amani. Hujawa na wasiwasi kwamba yumkini umeitelekeza familia. Haachi
kukupigia simu kuuliza lini utarudi.
9. Anaheshimu ndoa yako na haingilii mambo yenu: Hamuulizi
mwanaye au yeyote kuhusu mambo ya ndoa yenu. Anajiweka mbali lakini
tatizo likitokea, anakuwa wa kwanza kuja kuwasaidia.
10. Anakuona kuwa ni chaguo sahihi: Mara
nyingi mwanaume ndiye anayefanya uamuzi wa kuoa. Lakini, anapomchagua
mtu, mama hulazimika kukubali. Mama mkwe anayekupenda huamini kwamba
wewe bado ni chaguo sahihi hata kama miaka mingi imepita tangu
ulipoolewa. Hizo ni ishara zitakazokuonesha kuwa mama mkwe anakupenda au
la!.
COMMENT AND SHARE...................!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!