FAHAMU Namna ya Kuishi na Mpenzi Anayependa Fedha…:;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na
mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika
mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana.
Suala la kusaidiana si
la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni
kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale
ambao wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha!
Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana
kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo
linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo
sababu ya kuachana.
Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto
na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba
mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana
kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani
nakichuna kama sina akili nzuri.”
Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si
hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani
wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila
kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama
watajishughulisha.
Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano
wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa
kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini,
hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.
Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na
shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna
mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia.
Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba
ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati
hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili.
Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta
kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba
mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai,
baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako
ana fedha au laah.
Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka?
Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye
tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine
ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende
tukaone.
MWELEZE UKWELI Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba,
mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda
ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara
nitakununulia hiki na kile.
Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna
wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke
akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.
JENGENI KUSAIDIANA Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi
wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta
kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake
ana kazi yake.
Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi
wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi
na ataweza kubana matumizi.
ACHA UFUJALI Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni
wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza
kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!
Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha
itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa
ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri
kumbe ni kapuku tu.
BAKI NA HILI Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si
kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku
na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.
Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero.
Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo
epukana na tabia hiyo.
COMMENT AND SHARE..........................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!