Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE – JKCI iliyopo Jijini Dar es
salaam kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya APOLLO
ya nchini INDIA imefanikiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo Sita
bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, mmoja wa madakta wa taasisi hiyo
Dkt. BASHARI NYANGASA amesema kuwa upasuaji huo umesahidia kupunguza
madhara ambayo yangetokana na kutumia mashine hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tiba ya moyo Dkt. PETER KISENGE amesema
kuwa upasuaji wa aina hiyo ni ni endelevu na kutoa wito kwa madaktari
wote nchini kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo ya moyo katika taasisi
hiyo ili wakapatiwe matibabu.
Upasuaji huo kwa wagonjwa wa moyo SITA ndani ya nchi umeisaidia
serikali kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 170 ambazo zingetumika endapo
wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!