Rais
wa zamani wa nchi ya Ureno, Mario Soares ambaye anaheshimika kama baba
wa demokrasia nchini humo amefariki dunia hapo jana akiwa na umri wa
miaka 92.Rais
huyo wa zamani ndiye mwanzilishi wa chama cha kisoshalisiti nchini humo
na katika kipindi cha uhai wake alitumia miongo kadhaa katika masuala
ya siasa ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele wakati wa mchakato wa
nchi hiyo kujiunga kwenye Umoja wa Ulaya.Soares
alikuwa rais wa nchi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 1986 hadi
mwaka 1996 baada ya kuwa tayari amelitumikia taifa hilo katika nyadhifa
za uwaziri wa mambo ya nchi za nje na Waziri Mkuu.Ureno imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatatu kwa ajili ya kuomboleza kifo cha kiongozi huyo.
COMMENT AND SHARE.........!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!