Waziri mkuu MAJALIWA asema hataruhusu wanasiasa kusababisha vurugu:;
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Serikali itahakikisha inalinda amani
iliyopo nchini gharama yoyote ile na kamwe haitoruhusu mwanasiasa
yeyote
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema Serikali itahakikisha inalinda
amani iliyopo nchini gharama yoyote ile na kamwe haitoruhusu
mwanasiasa yeyote kusababisha vurugu zitakazochochea uvunjifu wa amani.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa dini
pamoja na wazee wa mkoa wa RUKWA baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara
ya kikazi ya siku mbili.
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amesema serikali inataka Watanzania
waweze kufanya kazi zao zinazowaingizia kipato na kuwaletea tija katika
hali ya utulivu hivyo suala la kudumisha amani ni muhimu kwani vurugu
zikitokea hawatakuwa na mahali pa kukimbilia
Waziri Mkuu amewataka viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa
pamoja na viongozi wake kwa sababu kazi ya uongozi ni ngumu na ina
changamoto nyingi.
Hali kadhalika Waziri Mkuu MAJALIWA amewaagiza viongozi wa dini wa
mkoa wa RUKWA kuharakisha uundwaji wa Kamati ya Amani ya mkoa huo.
Naye Sheikh wa mkoa wa Rukwa, Rashid Akilimali amesema madhehebu ya
dini hayawezi kuvuruga amani ya nchi ila anahofu na baadhi ya viongozi
wa vyama vya siasa kutokana na vitendo vyao vya kuhamasisha vurugu.
Kwa upande wake Katibu wa Wazee mkoani Rukwa, Kanali Mstaafu, JOHN
MZURIKWAO amemuomba waziri mkuu kuwasaidia kutatua kero mbalimbali
zinazoukabili mkoa huo zikiwemo za malipo ya pembejeo kwa mawakala wa
kilimo pamoja na mgogoro wa Ardhi katika shamba ya Efatha.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!