
Walimu 22 wa Shule ya Sekondari ya Azania Manispaa ya Ilala, akiwamo
Mwalimu Mkuu, wamehamishwa kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na matokeo
mabaya ya kidato cha sita.
Chanzo hicho cha habari kiliongeza kuwa kati ya walimu hao, 17 walikuwa
wanafundisha kidato cha tano na sita huku wanne kidato cha kwanza hadi
cha nne na mmoja aliyekuwa mkuu wa shule hiyo.
Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya walimu 17, wengi wao walikuwa
wanafundisha mchepuo wa ECA ambao wote wamehamishwa na kupangiwa shule
nyingine huku wengine wakihamishiwa shule za kata na kupangiwa
kufundisha kidato cha kwanza, pili na tatu. Awali, walimu hao walikuwa
wakifundisha kidato cha tano na sita.
Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo
ya kidato cha sita na shule hiyo kongwe ikajikuta imo katika kundi la
shule 10 za mwisho zilizokuwa na matokeo mabaya.
COMMENT LIKE AND SHARE.......................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!