Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, ZEID RAAD AL HUSSEIN ameitaka ETHIOPIA kuwaruhusu wachunguzi wa kimataifa
Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, ZEID RAAD AL
HUSSEIN ameitaka ETHIOPIA kuwaruhusu wachunguzi wa kimataifa kufanya
uchunguzi kuhusiana na kuuawa kwa waandamanaji 100 katika majimbo ya
OROMIA na AMHARA wiki iliyopita .
ZEID amesema madai ya matumizi ya silaha za moto wakati wa maandamano
hayo ni lazima yafanyiwe uchunguzi na kuongeza kuwa ofisi yake
inafanya mazungumzo na serikali ya ETHIOPIA kufuatia vifo hivyo.
Aidha amesema ofisi yake haijaona jitihada zozote zikichukuliwa
kufanya uchunguzi tangu maandamano hayo yalipoanza kufanyika kwenye
majimbo hayo mwezi Januari mwaka huu.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!