Kampuni ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja na
mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya
Rio 2016 yaliomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika
nafasi ya 5 kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume.
Katika Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania imemzawadia
Alphonce Simbu shilling za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa kila
mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika
maandalizi yake ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP
yanayotarajiwa kufanyika mjini London Uingereza August 2017.
Vile vile bwana Alphonce Simbu atapatiwa vifaa maalumu vya
kuumuwezesha kufanya mazoezi yake vyema. Vifaa hivi ni kama vile, viatu
na nguo za mchezo wa Riadha.
Si hivyo tu bali Kampuni ya MultiChoice itamtengenezea makala yenye
kuonyesha matukio mbalimbili aliyopitia ya Kimichezo na Familia siku za
nyuma. Vile vile watarekodi mazoezi atakayo anafanya akiwa katika kambi
ya riadha Chuo cha Wakala wa Mistu Fiti kilichopo West Kilimanjaro eneo
la Ngarenairobi Wilaya ya Sia Mkoa Kilimanjaro.
Makala hii itarushwa kwenye DStv hapo baadae.
Katika Kipindi cha
hicho cha mkataba huu Alphonce Felix Simbu atakuwa Balozi wa Kampuni ya
MultiChoice Tanzania ambapo atashiriki katika promosheni mbalimbali
kutangaza huduma zake.
Alipokuwa akisaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice
Tanzania Maharage Chande mbele ya Rais wa Riadha Tanzania na mkuu wa
mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, mwalimu wa wake Alphonce Nd. Francis John
Marcially pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Furaha
Samalu, alisisitiza kuwa “huu ni mwanzo na kadri mafanikio yanavyo
ongezeka Multichoice itakuwa tayari kuwa mstari wa mbele kushirikiana na
chama cha riadha Tanzania katika kunyanyua riadha Tanznaia na kurudisha
heshma ya taifa kwenye mchezo huo”.
COMMENT AND SHARE...................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!