Meneja wa klabu ya Arsenal ya
Uingereza, Arsene Wenger ameiambia BBC kuwa hatma yake katika klabu
hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu hiyo msimu huu
yatakavyokuwa.
''Mkataba wangu utakamilika Juni mwakani kwa hivyo
nitakachofanya baada ya hapo itategemea na matokeo ya msimu huu''
alisema Wenger.
Raia huyo wa Ufaransa 66, aliajiriwa mwezi Septemba 1996 kuiongoza klabu hiyo.
Mkataba wake wa sasa utakamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka ujao.
Arsenal
haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004 jambo
ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa mashabiki wa
klabu hiyo.
Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhfa wa kocha
wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuchukua pahala
pake Roy Hodgson.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!