Watu watano wamefariki dunia na wengine 54 wamejeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Leonard Nyandahu amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 3, 2022 majira ya Saa 8 usiku, ikihusisha basi kampuni ya Super Najimunisa likitokea Dar es salaam kuelekea Jijini Mwanza, na lori likitokea Mwanza kwenda Dar es salaam likiwa na mzigo wa dagaa.
Nyandahu amesema chanzo cha ajali hii ni uzembe wa dereva wa basi kwa kutozingatia vibao vya usalama barabarani na kuendesha mwendokasi.
Akieleza jinsi ajali hiyo ilivyotokea, abiria aliyenusurika, Fred Mahina amesema dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha mwendokasi na walipokuwa wakimzuia aliwajibu wangetaka usafiri wa raha wangepanda ndege, huku akiwaambia wasali sana ili wafike salama.
"Baada ya kuona mwendo kasi, tulimwambia dereva hakutusikia, tulipofika Morogoro dereva akiwa mwendokasi alikwaruza lori tukapona kuanguka, lakini akazidi kuendesha mwendokasi.
“Abiria tulipokuwa tukipiga kelele apunguze mwendo, aligoma na kutuambia tusali, ndipo tulipofika hapa Shinyanga na kupata ajali," anasema Mahina
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Dk Luzila John amethibitisha kupokea vifo vya watu watano pamoja na majeruhi 54 ambao wanaendelea na matibabu.
Amesema watu hao ambao wamepoteza maisha bado hawajatambuliwa majina yao, na wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitalini hapo na majeruhi wanaendelea kuhudumiwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!