Aje ni wimbo wa Alikiba uliompa mafanikio makubwa mwaka jana ikiwemo
tuzo kadhaa za video bora ya mwaka ikiwemo ile ya Soundcity MVP Awards.
Baada ya kuwepo version yenye verse toka kwa rapper Jude ‘M.I’ Abaga aka
Mr Chairman wa Nigeria iliyovuja hata kabla ya official video,
mashabiki walikuwa wamekaa tamaa kuwa hakutokuwepo na official remix
yake.
Habari njema ni kuwa, Alikiba anaileta remix official ya Aje. Na tena itakuwa ni video.
“Ndio, remix inayokuja ndio ambayo yuko M.I na ina utofauti than the one
that leaked,” meneja wa Alikiba, Seven ameyasema hayo. Seven amewataka
mashabiki wawe tayari muda wote sababu remix hiyo itaachiwa kwa
kushtukiza.
“He will just release it when it’s ready,” ameongeza.
“Hatutoi official release date. It will drop unexpectedly.”
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!