Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Amina Hassan (34) Mkazi wa Mtaa wa Lukilini, Kata ya Kalangalala, mkoani Geita amefariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo baada ya kuchomwa visu zaidi ya mara 10 katika sehemu mbalimbali za tumbo na kifuani.
Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Agosti 31, 2022, inaelezwa kuwa alifanyiwa unyama huo na mumewe aitwaye Mashaka Jeremia (46) Mzaliwa wa Kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita.
Baada ya kutekeleza unyama huo, mtuhumiwa aliefanya tukio hilo alikimbia na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Dkt. Mfaume Salum amethibitisha kufariki kwa mwanamke huyo na kwamba walimpokea Agosti 31 saa sita usiku akiwa amejeruhiwa.
Marehemu Amina ameacha watoto wawili huku chanzo cha tukio hilo kikiwa hakijafahamika bado.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!