Club ya AFC Bournemouth ya England ikiwa zimepita siku tatu toka wapoteze kwa kipigo cha kihistoria kwa kufungwa magoli 9-0, leo wamefikia maamuzi ya kumfuta kazi Kocha wao Mkuu Scott Parker baada ya kuingoza timu hiyo katika michezo minne ya Ligi Kuu England.
Scott Parker katika michezo yake minne ya Ligi Kuu England aliyoiongoza Bournamouth hadi sasa ameshinda mchezo mmoja 2-0 dhidi ya Aston Villa na baada ya hapo vilifuatia vipigo vitatu mfululizo dhidi ya Liverpool walifungwa 9-0, dhidi ya Arsenal walifungwa 3-0 na dhidi ya Man City walifungwa.
Huenda Bournamouth wameamua kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka au kujiondoa katika hatari ya kushuka daraja, japokuwa wengine wanaamini maboss wamekuwa na presha Bournamouth ameanza na ratiba ngumu kwa kucheza na vigogo, hadi sasa Bournamouth wana point 3 na Waco nafasi ya 17.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!