Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

Paul Pogba; Wanafanya Njama Niwape Pesa, Kaka Yangu Anahusika Pia

 




KUFUATIA maneno ya kaka mkubwa wa kiungo wa kati wa Ufaransa na klabu ya Juventus Paul Pogba, Mathias Pogba    siku kadhaa zilizopita, akidai hivi karibuni ataweka wazi ukweli wa mambo anayoyafanya kiungo huyo na kuwaonesha mashabiki wake sura halisi ya staa huyo wa Juventus.

 

Paul Pogba ameripotiwa kuwaambia polisi kuwa kaka yake huyo mkubwa Mathias Pogba pamoja na rafiki zake wengine wa zamani wamekuwa wakifanya njama za kumfanya mchezaji huyo awape pesa kwakutumia vitisho vya aina mbalimbali ikiwemo hilo la kaka yake huyo kutishia kuweka hadharani mambo anayoyafanya mchezaji huyo.

 

Pogba ameweka wazi kuwa hakuna chochote kibaya ambacho amekifanya na kudai ya kuwa anachokifanya kaka yake huyo ni katika njama za yeye na baadhi ya rafiki zake kumfanya awape pesa. Tayari jambo hili lipo mikononi mwa polisi wakilifanyia uchunguzi.


Hakuna chochote kibaya nilichofanya, wanataka niwape pesa

Pogba amewaambia polisi kwamba alivamiwa na majambazi wawili waliokuwa na silaha ambao walidai euro milioni 13 kutoka kwake. Genge hilo lilimshutumu mchezaji huyo nyota kwa kuwatelekeza mara tu baada ya kupata umaarufu.


Wananishutumu kuwatelekeza baada ya kupata umaarufu

Pogba amesema zaidi kwamba watu hao walijaribu kumshinikiza kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu Kylian Mbappe. Kwa mujibu wa Pogba, anasema wamlitishia kueneza habari kwamba Pogba alikuwa akimfanyia uchawi mchezaji mwenzake huyo wa kimataifa wa Ufaransa jambo ambalo Pogba amelikataa.

 
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube