bikra ni nini?
hii ni ngozi laini sana inayofunika
uke kwa wanawake ambao hawajawahi kushiriki ngono kabisa, kikawaida
mwanamke anaacha kuitwa bikra pale ngozi hii inapoondolewa.... ngozi hii
kitaaamu inaitwa hymen.
hymenorrhaphy ni nini?
huu ni upasuaji unaofanyika kuirudisha bikra ya mwanamke ambayo imeshatoka tayari kwa sababu mbalimbali.
aina hii ya upasuaji mara nyingi
hazipatikani kweye hospitali za kawaida kwani hazina umuhimu wowote
kwenye matibabu na zinaweka kwenye kikundi cha plastic au cosmetic
surgery,hivyo mara nyingi hufanyika kwenye hospitali au clinic binafsi
na mabingwa wa magonjwa ya akina mama yaani gynacologist..
idadi ya wanawake wanaofanyiwa aina
hizi za upasuaji inazidi kuongezeka miaka inavyozidi kwenda mbele
kutokana na watu kuanza ngono mapema sana.
watu gani wanatakiwa wafanyiwe aina hizi za upasuaji?
wanawake ambao wanataka kurudisha
bikra zao ambazo zimeshatoka wanatakiwa kufanya upasuaji huu kwani
hakuna dawa yeyote inayoweza kurudisha bikra na ukiisikia ujue ni
utapeli.
katika hali ya kawaida bikra inaweza
kutoka kwa kushiriki ngono, kupata ajali na kuumia, tabia ya kujichua,
mazoezi kama kuendesha baiskeli au farasi, matumizi ya aina fulani za
pedi au magonjwa fulani fulani.
wakati mwingine ngozi ila ya bikra
inaweza kua ngumu sana kiasi kwamba ikakataa kuchanika hata kwa
kuingiliwa kingono. hivyo mwanamke kutotoka damu wakati wa ngono kwa
mara ya kwanza haimaanishi kwamba mwanamke sio bikra.
kwanini wanawake wanafanya aina hizi za upasuaji?
wanawake hua wanasababu mbalimbali kama ifuatavyo
1 kuwaonyesha wanaume zao au
jamii zao kwamba wao ni mabikra kipindi cha ndoa hasa kwenye jamii
fulani fulani ambazo bikra ni muhimu sana siku ya ndoa.
2 kuwasaidia wenye maumivu ya kisaikolojia baada ya kubakwa, hii inawafanye wapate amani kidogo baada ya upasuaji huu.
3 kurudisha bikra ambayo imeharibika sababu ya kuumia kwa ajari.
upasuaji huu unafanyikaje?
hii ni aina ya upasuaji mdogo ambayo
inafanyika kwa kuchoma sindano ya ganzi tu na wala haihitaji kwanamke
kupewa dawa za usingizi, japokua kuna wakati mwingine kutokana na
mazingira ya mgonjwa daktari anaweza kulazimika kutoa dawa ya usingizi.
kuna aina tatu za upasuji za kurudisha bikra kama ifuatavyo.
1 kuishona tena ngozi ile ya ya
hymen ambayo inamfanya mwanamke aitwe bikra kwa kuirudisha pamoja na
kuiacha ipone kisha kurudi kama zamani
2 kuweka ngozi ya hymen ya bandia
na kuishonea pale kisha kuweka ndani yake aina fulani ya kimiminika
kinachofanana kabisa na damu ili damu ionekane ikitoka wakati wa ngono
3 kuikata ngozi ya hymen ambayo ilichanika mwanzoni na kuitoa nje kisha kuirudishia upya na kuishona kabisa kama mwanzo.
wanawake wanaofanya aina hii za
upasuaji wanatakiwa wafahamu kwamba wanatakiwa wakae bila kushiriki
ngono wiki tatu mpaka miezi mitatu ili bikra ishike vizuri hivyo ni
vizuri kuifanya mapema kabla ya ndoa sio unataka ufanyiwe leo afu wiki
ijayo uolewe.
nyuzi zinazotumika kushona ngozi ile ya bikra hua haziondolewi yaani baadae huyeyuka ndani kwa ndani.
madhara ya upasuaji huu
upasuaji huu ni salama kabisa ila hua una madhara madogo madogoambayo ni kawaida hata kwa uparesheni zingine kama ifuatavyo.
kutokwa damu; hii ni kawaida hata kwa uparesheni zingine lakini damu hii inatakiwa ikauke na kuondoka baada ya siku chache.
kubana sana; wakati mwingine daktari
anaweza akaishona ngozi ile na kuibana sana kiasi kwamba ikawa ngumu
sana siku ya kuitoa wakati wa kushiriki ngono. hua na maumivu makali
ambayo huisha bila dawa yeyote baadae.
infection; hii husababishwa na
kushambuliwa na bacteria baada ya upasuaji lakini huweza kuzuiliwa kwa
kupewa dawa za kuzuia hali hii mfano antibiotics
mwisho; aina za upasuji hizi
zinapatikana nje ya nchi kwa wingi, kwa nchini tanzania na afrika kwa
ujumla zipo pia lakini ni sehemu chache sana.
dunia inakwenda kwa kasi sana hivyo mwanaume ukijikuta umeoa bikra mwenye watoto wanne usishangae...
COMMENT AND SHARE...............!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!