Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment and dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!! Welcome to VIVAX MEDIA, feel free to Comment., dont forget to Share (also please Click on the YOUTUBE, YOUTUBE, YOUTUBE button above/bellow the page).....!!

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA VYETI VYA WAHITIMU WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU ZA AFYA, MIFUGO NA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 SASA;



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini.

NACTE ina wajibu wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wenye sifa stahiki kwa mafunzo ya programu za Afya, Mifugo na Ualimu yanayozingatia umahiri.



Tarehe 14 Julai 2017 Baraza lilitoa taarifa kwa umma kuwa vyeti vya wahitimu wa mafunzo ya programu za Afya, Mifugo na Ualimu wenye sifa stahiki kwa mwaka wa masomo 2015/16 vingeweza kutolewa muda wowote ndani ya Mwezi wa Julai 2017. Kwa sababu za kiufundi, vyeti hivyo havikutolewa kama ilivyoahidiwa. Hata hivyo, Baraza linatarajia kuwa vyeti vitakuwa tayari ifikapo tarehe 12 Agosti 2017.



Kuhusu uthibitisho wa wanafunzi kuhitimu mafunzo ya taaluma husika, wahitimu wanashauriwa kuomba ‘transcripts’kupitia tovuti ya NACTEwww.nacte.go.tz na transcripts ni uthibitisho halisi wa uhitimu wa mwanafunzi. Baraza linaendelea na zoezi la utoaji wa transcript kwa wahitimu wote kulingana na maombi yanavyowasilishwa.





COMMENT AND SHARE.. .!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!

Comments

Facebook Twitter Youtube