MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana
amecheza vizuri kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikilazimisha
sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Lokeren Uwanja wa Daknam mjini Lokeren,
Ubelgiji kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya
UEFA Europa League mwakani.
KRC Genk walitangulia kwa bao la penalti la kiungo mkongwe wa umri wa
miaka 33, Mbelgiji Koen Persoons aliyejifunga dakika ya nne, kabla ya
mshambuliaji mwenye umri wa miaka 31, Mbelgiji pia Tom De Sutter
kuisawazishia Lokeren dakika ya 57.
Pamoja na sare hiyo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa
kuwania tiketi ya Europa League mwakani kwa kufikisha pointi 26 baada ya
kucheza mechi tisa na Samatta jana ameichezea Genk mechi ya 58 tangu
ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga
mabao 19.
Kati ya mechi hizo 58, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 40
msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 36 tu ndiyo alianza, 10 msimu
uliopita na 26 msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu
huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita
msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu
uliopita.
Kikosi cha Lokeren kilikuwa: Verhulst, Skulason, Single, De Sutter/Enoh
dk65, Terki, Huppert/Rocketman Stra dk76, Ticinovic, Rassoul/Martin
dk63, Miric, Knight na Monsecour.
KRC Genk : Ryan, Nastic, Wouters, Seigers, Castagne, Berge,
Kumordzi/Heynen dk61, Sabak/Writers dk76, Naranjo, Buffalo/Vermijl dk45
na Samatta.
COMENT AND SHARE..............................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!