Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema utata kuhusu hatima yake katika klabu hiyo huenda ulichangia
kushindwa kwa klabu hiyo kumaliza katika nafsi nne za kwanza katika Ligi
Kuu ya England.
Hata hivyo, amesema hakuna anayeweza kutilia shaka kujitolea kwake kufanya kazi yake katka klabu hiyo.
Imekuwa
ni mara ya kwanza kwa Arsenal, waliomaliza wa tano, kukosa kufuzu kwa
Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika kipindi cha miaka 20.
Wenger,
ambaye mkataba wake unamalizika majira yajayo, hivi majuzi alisema
hatima yake itaamuliwa baada ya fainali ya Kombe la FA mnamo 27 Mei.
"Nimekataa klabu zote zilizonitafuta kutoka pande mbalimbali duniani," Mfaransa huyo wa miaka 67 alisema.
Wenger
amekuwa kwenye usukani Gunners tangu 1996 ambapo ameshinda mataji
matatu ya Ligi ya Premia na Vikombe sita vya FA, lakini mashabiki wa
Arsenal msimu huu wamekuwa wakimtaka ajiuzulu.
"Ninamini tangu Januari tumecheza katika mazingira magumu sana kwa sababu mbalimbali," aliongeza.
"Baadhi
yenu mnajua hilo na hilo ni jambo ngumu sana kwa wachezaji - na kuna
baadhi ya sababu ambazo tutazizungumzia siku nyingine.
"Kiakili,
hali ilikuwa ngumu sana. Mambo yamekuwa magumu, ndio, na bila shaka hali
yangu imechangia hilo lakini huwezi kutilia shaka utaalamu wangu au
kujitolea kwangu."
Arsenal walilaza Everton 3-1 Jumapili lakini kwa sababu Liverpool
walilaza Middlesbrough, Gunners walimaliza alama moja nyuma ya klabu
hiyo ya Jurgen Klopp iliyomaliza nafasi ya tano.
Wenger, ambaye
klabu yake itakutana na mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea katika
fainali ya Kombe la FA alisema inasikitisha sana kwamba Arsenal
haitakwua ikicheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Aliongeza: "Tulifanya kazi yetu kwani wewe ni mtaalamu na sehemu ya
kazi yako kama mtaalamu ni kuendelea kufanya kazi kama mtaalamu hata
mazingira yanapokuwa magumu."
Wenger atetewa na Ferguson
Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye mara
kwa mara walikuwa na uhasama na Wenger alipokuwa Old Trafford, ambapo
alishinda mataji 13 ya Ligi amemtetea Wenger.
Ferguson alikuwa mkufunzi Man Utd kwa miaka 26 naye Wenger sasa yupo Arsenal kwa mwaka wake wa 21.
"Kwa
sasa, bila shaka, ukizingatia presha ya kushangaza ambayo Arsene
anakabiliwa nayo, nashangaa iwapo huwa wanatambua kazi nzuri ambayo
amewatendea," Ferguson aliambia Sky Sports.
"Jambo zuri zaidi
kumhusu ni kwamba; amefanikiwa kujitoa kwenye kichaka hicho cha lawama
kwa miezi kadha sasa, na hajawahi kusalimu amri. Amepitia mengi,
ameonesha kujitolea kwake, na ukakamavu fulani. Nafikiri ukiangalia
hilo, ustadi na kiwango chake, sina uhakika kwamba watawahi kumpata
meneja mwingine kama yeye.
COMMENT AND SHARE..............................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!