Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wazuri sana wakati wa mechi
dhidi ya Manchester City ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 uwanjani
Emirates.
Amesema hayo licha ya kwamba bado wapo mashabiki walioandamana kumpinga wakati wa mechi hiyo ya Jumapili.
Wenger,
ambaye anakabiliwa na shinikisho baada ya kushindwa mechi moja pekee
kati ya sita walizocheza karibuni amekuwa akitakiwa na baadhi ya
mashabiki ajiuzulu.
"Lazima niseme kwamba, licha ya yote
yaliyofanywa na baadhi ya mashabiki, mashabiki wetu walikuwa wazuri sana
leo," alisema Mfaransa huyo baada ya mechi.
Arsenal, ambao
wameshuka hadi nafasi ya sita kwenye Jedwali, walitoka nyuma mara mbili
kulazimisha sare hiyo dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola.
"Katika
nyakati ngumu sana, tukiwa 1-0 chini na 2-1 chini, wangetugeuka lakini
nafikiri walikuwa wazuri sana na walituwezesha kupitia vipindi hivyo
vigumu."
Mabao kutoka kwa Theo Walcott na Shkodran Mustafi cyalisaidia Arsenal kukomboa mabao kutoka kwa Leroy Sane na Sergio Aguero.
Wenger anaamini matokeo katika mechi hiyo yatawarejeshea Arsenal imani na kuwawezesha kurejelea ushindi wao kama zamani.
Mkataba wa Wenger unafikia kikomo mwisho wa msimu huu.
Ameahidiwa mkataba wa miaka miwili na alsiema mnamo Machi 18 kwamba atatangaza uamuzi kuhusu mustakabali wake hivi karibuni.
Kipa wa zamani wa ,Bob Wilson alisema kwamba Wenger anafaa kutangaza mustakabali wake "kwa maslahi ya klabu".
Lakini
Wenger Jumapili alisema: "Nimeonesha uzalendo na nimeendelea kujitolea.
Sijui nitakuwa hapa muda mgani lakini naipenda klabu hii na nitafanya
lililo njema Nitafanya hilo karibuni, msiwe na wasiwasi."
Arsenal wamo namabri sita katika Ligi ya Premia kwa sasa, alama saba nyuma ya Manchester City walio nambari nne.
Gunners watakutana na West Ham nyumbani Jumatano kisha wasafiri Crystal Palace Jumatatu.
COMMENT AND SHARE....................................!!!!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!