Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili wamefikishwa
katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi ya leo na kusomewa
mashitaka matatu yanayohsiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya
bangi.
Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali
Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii
huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi
cha gramu 1.08.
Akisoma Shtaka hilo linalowakabili
watuhumiwa wote watatu, mbele ya Hakimu Huruma Shaidi wa Mahakama hiyo,
Wakili wa Serikali Mtalemwa Kisenyi ameiambia mahakama hiyo kuwa siku ya
tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio Jijini
Dar es Salaam watuhumiwa hao watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa
hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya
kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.
Washtakiwa wote wamekana shitaka hilo,
kisha kuachiwa kwa dhamana ya shilingi Milioni 5 na kuwa na wadhamini
wawili kila mmoja huku uchunguzi ukiendelea ambapo kesi hiyo
itasikilizwa tena tarehe 22 mwezi wa pili mwaka 2017.
Kesi hiyo iko chini ya Hakimu Huruma Shaidi, na mwendesha mashitaka Mtalemwa Kishenyi
COMMENT AND SHARE.....................................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!