Nchi ya Urusi imesimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya
Riadha baada ya kubainika kwa wanamichezo wake kujihusisha na utumiaji
wa madawa ya kusisimua misuli.
Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa
Urusi wanaweza kushiriki na kushindana mahali popote endapo wanaweza
kukidhi vigezo vya vipimo.
Urusi ilisimamishwa na shirikisho la
riadha ulimwenguni I doubel AAF mwezi Novemba mwaka 2015, na
wanariadha wake kukosa kushiriki michuano ya Rio Olimpiki ya mwaka
jana.
Uingereza wanatarajia kuwa wenyeji wa mashindano ya riadha ya dunia kati ya Agosti 04-13 mwaka huu 2017.
Uamuzi wa kusimamishwa kwa Urusi umefanyika kupitia mkutano mkuu wa Baraza uliofanyika mjini Monaco .
COMMENT AND SHARE..................................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!