Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini leo wameondoka
rasmi Jijini DSM kuelekea mkoani DODOMA ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa
agizo la Rais JOHN MAGUFULI la kutaka wizara zote kuhamia mkoani
humo.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo JULIANA PALLANGYO amesema kuwa hii ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo.
PALLANGYO pia amewapongeza wafanyakazi wote waliokubali kuhamia
mkoani DODOMA bila malalamiko na kuahidi kuwa shughuli zote za kikazi
zitaendelea kama kawaida.
Hatua ya wizara mbalimbali kuhamishia ofisi zake mkoani DODOMA
inafuatia agizo lililotolewa mwaka 2016 na Rais JOHN MAGUFULI la
kuzitaka Wizara zote kuhamia mkoani humo mpaka ifikapo februari 28
mwaka huu.
COMMENT AND SHARE.............................!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!