Mchungaji Anthony Lusekelo amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa
pombe, na kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa 'wine' isiyo na
kilevi, huku akisita kusema endapo unywaji pombe ni dhambi au siyo
dhambi.
Amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na
kuweka wazi kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa
ushahidi juu ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi
ama usiwe dhambi kulingana na imani na dini ya mtu.
"Hao wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa,
nilikuwa nakuywa wapi na aliyeniona ni nani... kuna sehemu nyingine
pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar".
Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi?
Hilo ni swali lingine alilokutana nalo kuhusu unywaji Pombe, ambapo
katika majibu yake amesema hawezi kusema kama ni dhambi au lah, maana
inategemea na imani ya mtu, huku akiongeza kuwa Bibilia haijazuia
unywaji pombe
"Inategemea na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi
ni makubaliano yenu kwenye dini yenu. Bibilia inasema kula kitu
chochote hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa
pombe ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biliblia haijaandika moja kwa moja
kwamba msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna
ufisadi, cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu"
Ikumbukwe kuwa sekeseke lililosababisha Mzee wa upako adaiwe kunywa
pombe, lilihusisha kurushiana maneno na jirani zake ambapo baada ya hapo
vyombo vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo
Mzee wa Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo
waandishi walioandika habari hiyo.
Alipoulizwa kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo, alisema
kuwa tayari amewasamehe ingawa uwezo wa kuwaombea kifo anao.
"Tulisema hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa
sababu sisi ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni
bora kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao,
lakini nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua
kusamehe"
Baadhi ya watu walitaka kujua ni kwanini haendi kuombea wagonjwa
hospitalini ili wapone, ambapo alijibu kuwa maombi hufanywa katika
mazingira maalum, na kwamba hospitali kila mgonjwa ana imani yake.
"Maombi lazima kuandaa mazingira, na sehemu ambayo Mungu amesema
tukutane ni kanisani, ndiyo maana hata wakati wa Yesu wagonjwa ndiyo
walimfuata Yesu, siyo Yesu aliwafuata wagonjwa.. Kinachoponya ni imani
ya mtu, pale hospitali kila mtu ana imani yake, wakati mwingine hata
kumuombea mtu inabidi umuombe kwanza maana wengine hawapendi kuombewa".
COMMENT AND SHARE............................!!!!!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!