NEW DELHI, INDIA: WANAWAKE wawili, Mzambia Thelma Mkandawire (38) na
Mtanzania Pamela David Kiritta (41) wamekamatwa kilo nne za madawa ya
kulevya (cocaine) yenye thamani ya Rs milioni 300 sawa TZS bilioni 9.7
katika hoteli moja karibu na uwanja wa ndege wa New Delhi nchini India.
Askari wanaohusika na kupiga vita madawa hayo nchini humo (NCB),
waliwatia mbaroni baada ya kudokezwa na hivyo kuanza kumfuatilia
Mkandawire aliyetua nchini humo kutokea Sao Paulo (Brazil) kupitia Addis
Ababa (Ethiopia) ambapo walimvamia akiwa hotelini eneo la Mahipalpur
akiwa na Kirrita aliyedaiwa kwenda kuupokea mzigo huo.
Mkurugenzi wa NCB wa Kanda ya Delhi, Madho Singh, alisema madawa hayo
yalipatikana katika mizigo ya Thelma na hivyo wanawake wote wawili
wamekamatwa kuhusiana na madawa hayo ambayo thamani yake katika soko ni
kubwa.
Habari nyingine zilisema kwamba Thelma aliwahi kukamatwa nchini Pakistan
mwaka 2015 akiwa na madawa ya kulevya lakini aliweza kuachiliwa kwa
madai ya kutoa hongo. Pia habari zimesema Kiritta alikuwa akikaa
katika nyumba moja eneo la Vasant Kunj la Delhi Kusini tangu aingie
nchini India mwanzoni mwa Januari mwaka huu.
Pamela ambaye hiyo ilikuwa ni safari yake ya tisa kwenda India, alikuwa
aupokee mzigo ambapo walivamiwa na askari na kupekuliwa begi lao
walikokuwa nalo na kukutwa na madawa hayo waliyokuwa wameyaweka
kitaalam kiasi kwamba mashine za uchunguzi zilishindwa kuyagundua
kutokana na kufungwa kitaalam.
Inasemekana madawa hayo yangefungwa katika paketi ndogondogo na kusambazwa kwa watumiaji nchini India.
Alipoulizwa, Kiritta alikiri kuingia nchini India mara tisa tangu 2006
na amewahi kwenda katika nchi nyingine za Ecuador na Kenya kwa shughuli
kama hizo.
COMMENT AND SHARE....!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!