Kampuni ya simu ya Blackberry inaishtaki Nokia kuhusu madai kwamba kampuni hiyo ya Finland imetumia uvumbuzi wake bila ruhusa.
Madai hayo ya ukiukaji yanahusisha teknolojia inayotumika katika 4G pamoja na mitandao mingine ya simu.
Kampuni hiyo ya Canada inadai kwamba transmita za Nokia pamoja na programu nyengime zinatumia teknolojia yake.
Nokia imeambia BBC kwamba inaliangazia swala hilo.
''Tunajua
kwamba kuna malalamishi ,tutayajadili madai yaliotolewa na kuchukua
hatua zinazohitajika kutetea haki zetu'',alisema msemaji.
Kesi hiyo inasikizwa nchini Marekani.
Blackberry inataka
kulipwa fedha badala ya kuizuia Nokia kutumia teknolojia yake kulingana
na nakala za mahakamani zilizochapishwa na tovuti ya habari ya Ars
Technica.
Madai hayo ni pamoja na yale yanayosema kwamba Nokia
ilikuwa inajua uwepo wa uvumbuzi huo baada ya kujaribu kuununua hapo
awali kabla ya Blackberry kuamua kutumia.
Kampuni hizo mbili
zilizozana 2012 wakati Nokia ilipojaribu kuhakikisha kuwa mauzo ya simu
za Blackberry yanapigwa marufuku nchini Marekani na Uingereza katika
mzozo mwengine. Kampuni zote mbili zimesitisha utengenezaji wa simu zao na badala yake
wametoa leseni za haki ya umiliki wa simu zao kwa kwa watengenezaji
wengine wa simu.
COMMENT AND SHARE................................!!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!