Bastian Schweinsteiger hataihama
klabu ya Manchester United na atajumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo
kinachocheza ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, kwa mujibu wa meneja
Jose Mourinho.
Kiungo huyo wa kati wa miaka 32 alifunga wakati wa ushindi wa United wa 4-0 Kombe la FA dhidi ya Wigan Jumapili.
Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuanza mechi katika klabu hiyo tangu Januari 2016.
Schweinsteiger
aliachwa nje ya kikosi cha Europa League msimu huu na Mourinho na
akalazimishwa kushiriki mazoezi na kikosi cha wachezaji wasiozidi umri
wa miaka 23 mwanzoni mwa msimu.
Mourinho amesema mchezaji pekee ambaye huenda akaondoka mwezi huu ni Ashley Young.
"Ataenda
kucheza Europa League kwa sababu tumeachwa na nafasi za kujaza kutokana
na kuondoka kwa [Memphis] Depay na [Morgan] Schneiderlin."
Schneiderlin aliuzwa Everton mnamo 12 Januari, naye Depay akajiunga na Lyon siku nane baadaye.
United
watakutana na Saint-Etienne hatua ya 32 bora Old Trafford tarehe 16
Februari, na mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye.
COMMENT AND SHARE...............................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!