Rais wa awamu ya nne wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amepata
nafasi ya kukutana na mabilionea wawili wakubwa duniani akiwa ziarani
Davos nchini Uswisi.
Rais
Jakaya Kikwete alikutana na tajiria namba moja Afrika, Alhaji Aliko
Dangote kutoka nchini Nigeria na tajiria namba moja duniani, Bill Gates
kutoka nchini Marekani.
Viongozi
hao wamekutana nchini Uswisi katika Mkutano wa Dunia wa Uchumi (World
Economic Forum) wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo wa
uchumi wa dunia.
Mbali
na masuala ya uchumi, mkutano au kongamano hilo pia hujadili kuhusu
mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa sasa yamekuwa ni tishio kubwa kwa
viumbe mbalimbali.
Mkutano
huu huudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na asasi
nyingine za kuraia zikiwa na lengo la kuweka nguvu pamoja na kuifanya
dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!