NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Hamad Masauni ameonya kuwa watu wakiwemo wanasiasa wanaoeneza taarifa za
uongo za kuwepo kwa baa la njaa, ni kosa na wachukuliwe hatua ikiwemo
kukamatwa.
Masauni amesema bado kuna watu
wanajichukulia mamlaka ambayo sio yao na kueneza uongo kuwa kuna njaa
nchini, hilo ni kosa kwa kuwa kwa kueneza propaganda hiyo kunaweza
kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
“Hizo ni propaganda za watu
wasioitakia mema nchi hii ….. mtu anapofanya kosa lazima achukuliwe
hatua …… Jeshi la Polisi liangalieni hili,” alisisitiza.
Masauni alitoa onyo hilo wakati wa
ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana mkoani Rukwa ambako Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven alimhakikishia kuwa mkoa huo hauna njaa,
bali una ziada ya kutosha.
“Nyie wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa
(Zelothe) amethibitisha kuwa hakuna njaa mkoani hapa lakini sio hapa
tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia kuwa hawana njaa,”
alisema Naibu Waziri Masauni na kuongeza: “Sasa wapo wanasiasa uchwara
wanaeneza propaganda kuna njaa, sio mamlaka yao kutangaza kuwa kuna
njaa, kueneza uongo kama huo ni si sawa kwa kuwa kunaweza kusababisha
uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwemo
kukamatwa,” alisisitiza.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe
alimweleza Naibu Waziri Masauni kuwa hali ya kiusalama katika mkoa huo
ni shwari ambapo amani na utulivu umeshamiri kwa kuwa una chakula cha
kutosha.
COMMENT AND SHARE........................!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!