MESUT
Ozil ameamua kutuliza mzuka Arsenal na kutamka kuwa atasaini kandarasi
mpya ya kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Emirates kwa miaka mingi
ijayo.
Ozil
ambaye kwa sasa yuko nje ya dimba ameuambia mtandao wa Kicker wa
nyumbani kwao Ujerumani kuwa yuko tayari kusaini kandarasi mpya ya
kuendelea kuichezea Arsenal lakini kwa sharti la kuhakikishiwa kuwa
kocha wake Arsene Wenger ataendelea kuinoa klabu hiyo.
Mara
kadhaa Ozil ameshindwa kuficha hisia zake na kukiri kuwa aliamua
kuhamia Arsenal kwa sababu ya ushawishi wa Wenger hivyo kubaki kwake
Arsenal kutategemea kama kocha huyo Mfaransa atapewa kandarasi mpya.
Kauli
hiyo ya Ozil imekuja kama ahueni kwa mabosi wa Arsenal ambao kwa miezi
kadhaa sasa wamekuwa akipambana kumshawishi nyota huyo asaini kandarasi
mpya kabla ile ya awali haijafika mwisho mwaka 2018.
Wakati
huohuo Ozil amewataka watu mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wa
Arsenal akiwemo Thierry Henry kuacha kumuongelea vibaya kwani hawajui
kile kinachoendelea kati yake na Arsenal.
COMMENT AND SHARE..................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!