Darassa
Msanii mkongwe
wa bongo fleva, Prince Dully Sykes amesema wabongo wengi hawapendi
nyimbo zenye ujumbe wa kuhamasisha maendeleo, na ndiyo maana ngoma
nyingi zisizokuwa na ujumbe wa aina hiyo ikiwemo ya 'Muziki' ya Darassa,
huwa zina hit zaidi.
Dully alizungumza hayo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha Planet
Bongo cha EA Radio, alipokuwa akizungumzia mikakati yake kwa mwaka 2017
na kutakiwa kuelezea maana ya ngoma yake ya 'Inde' ambayo ilikuwa 'hit'
mwaka 2016.
Alisema
wimbo wa Darassa hauna ujumbe wowote wa kuhamasisha maendeleo isipokuwa
umejaa majigambo na kujisifia, na kwamba nyimbo za aina hiyo ndizo
hupendwa na watanzania huku akisema kuwa endapo Darassa angeimba
maendeleo, wimbo wake usingependwa."Kwani
wimbo wa darassa una ujumbe gani? siyo simba, siyo chui, hiyo si ni
kujisifia tu, wabongo ukiwaimbia eti sijui twende tukalime, tufanye kazi
maendeleo na vitu kama hivyo hawavipendi" Alisema Dully.Alisema
kwa kutambua hivyo, ndiyo maana na yeye hawezi kutunga nyimbo zenye
ujumbe wa maendeleo na ataendelea na ngoma kama ilivyo 'inde' na
nyingine ambazo zimetikisa anga la bongo fleva
Dully
Hata
hivyo, Dully alimpongeza Darassa kwa kazi nzuri na kwa kulishika game
la bongo kwa kipindi hiki, na kukiri kuwa kazi yake ni nzuri huku
akikataa kuwa ngoma ya Darassa haijamfunika kwa kuwa ngoma yake ya
'inde' ilikuwa hit kabla ya 'Muziki' ya Darassa.Kuhusu
ujumbe uliomo kwenye ngoma ya 'inde' Dully alisema ngoma hiyo
aliitengeneza kwa ajili ya kucheza kuburudisha zaidi maana hicho ndicho
watanzania wanachokipenda, huku akikanusha kuimba matusi na kusema
"Sijaimba matusi, ni jinsi wewe utakavyoutafsiri na kuuelewa, tuliza
akili yako utajua nimeimba nini, vitu vingine havisemwi hadharani"Kuhusu
mikakati yake ya mwaka 2017, Dully amesema muda si mrefu atatoa ngoma
nyingine ambayo anaamini itakuwa ni kali zaidi ya 'inde' na kuwataka
mashabiki wake wakae mkao wa kula.
COMMENT AND SHARE................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!