Wakili wa zamani wa haki za
kibinaadamu, Nana Akufo-Addo, ameapishwa kuwa rais mpya wa Ghana, katika
sherehe iliyohudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.
Katika hotuba
yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais anayeondoka madarakani,
John Dramani Mahama, kwa namna alivokiri kushindwa katika uchaguzi wa
mwezi uliopita.
Viongozi kadha wa Afrika walikusanyika katika mji
mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kutawazwa rais mpya, Nana
Akufo Addo.
Maelfu ya wageni walialikwa kwenye sherehe katika Medani ya Uhuru mjini Accra.
Bwana Akufo Addo, aliyewahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu,
alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada
ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo,
watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh,
anaondoka madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.
COMMENT AND SHARE............!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!