Klabu ya Chelsea ya Uingereza imepewa idhini na baraza la wilaya kujenga uwanja mpya mradi ambao utagharimu £500m.
Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kutoshea mashabiki 60,000.
Kamati
ya mpangilio wa wilaya ya Hammersmith na Fulham imeidhinisha mpango wa
kubomoa uwanja wa sasa wa Stamford Bridge unaotoshea mashabiki 41,000.
Miongoni
mwa yaliyomo kwenye mpango mpya wa ujenzi, ni pamoja na kujengwa kwa
njia ya kutumiwa na watu kutembea kutoka kituo cha reli kilicho karibu.
"Tunashukuru kwamba mpango wetu umeidhinishwa," Chelsea walisema kupitia taarifa.
"Uamuzi wa kamati hiyo hata hivyo hauna maana kwamba tunaweza kuanza
ujenzi mara moja. Hii ni hatua tu ya karibuni zaidi, ingawa ni hatua
muhimu sana, ambayo ilikuwa ni lazima tuitimize kabla ya kazi ya ujenzi
kuanza, pamoja na kupokea vibali vingine."
Meya wa London Sadiq Khan atakuwa na usemi wa mwisho kuhusu ujenzi wa uwanja huo mpya.
Ramani
ya uwanja huo mpya imechorwa na wasanifu mijengo Herzog na de Meuron,
ambao pia walichora uwanja wa Olimpiki wa "Birds Nest" mjini Beijing.
Mchoro wa uwanja mpya wa Stamford Bridge uliopendekezwa
Hatua ya kutolewa kwa idhini ya kujengwa kwa uwanja huo inamaanisha
kwamba sasa huenda Roman Abramovich akatafuta uwanja wa muda wa kutumiwa
na viongozi hao wa sasa wa Ligi ya Premia kwa karibu miaka mitatu
ujenzi utakapokuwa ukiendelea.
Viwanja ambavyo wanaweza kutumia ni Twickenham na Wembley.
Chelsea
huenda hata hivyo wakatatizika kuupata uwanja wa Wembley kwani
utatumiwa na wapinzani wao Tottenham Hotspur angalau kwa msimu wa
2017-18 wanapomalizia ujenzi wa uwanja wao wa kutoshea mashabiki 61,000.
Chelsea wanaweza bado kuendelea kutumia Stamford Bridge ujenzi ukiendelea, lakini mpango huo utakuwa ghali.
Mpango wa eneo ambalo uwanja mpya wa Stamford Bridge utajengwa pamoja na njia ya kutoka kituo cha treni cha Fulham Broadway
Abramovich amekuwa akitaka sana kupanua uwanja wa Stamford Bridge kwa miaka kadha sasa bila mafanikio.
Miaka
kumi iliyopita Arsenal walijenga uwanja wao wa Emirates unaotoshea
mashabiki 60,000. West Ham walihamia uwanja wao wa Olimpiki unaotoshea
mashabiki 57,000 eneo la Stratford, London mashariki na Spurs kwa sasa
wanapanua uwanja wao White Hart Lane.
Uwanja wa sasa wa Stamford
Bridge unaotoshea mashabiki 41,663 ndio wa saba kwa ukubwa miongoni mwa
viwanja vinavyotumiwa na klabu za Ligi ya Premia.
Uwanja wa Old Trafford unaotumiwa na Manchester United hutoshea mashabiki 76,000.
COMMENT AND SHARE..............!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!