Ni imani yangu kuwa uko salama rafiki na unaendelea vizuri katika
harakati zako za kila siku kuhakikisha unapata kile unachokitaka kwenye
maisha yako. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo ameweza
kutustahilisha tena kuiona siku hii ya leo. Kwa hiyo rafiki, tutumie
muda huu wa leo vizuri kwani leo ni siku bora ambayo haitokuja tena
kutokea katika maisha yetu hapa duniani.
Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo
tuweze kujifunza kwa pamoja yale ambayo nimeweza kukuandalia siku hii ya
leo. Hivyo basi, nakusihi ungana nami mwanzo hadi mwisho wa makala hii
ili tuweze kusafiri wote kwa pamoja. Leo tutakwenda kujifunza juu ya
madhara ya kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye kwenye maisha ya mahusiano.
Je ni madhara gani rafiki? Karibu rafiki tuweze kujifunza wote kwa
pamoja.
Katika moja ya matatizo yanayowasumbua watu duniani basi moja wapo ni
mambo ya mahusiano. Mahusiano haya yanaweza kuwa mahusiano ya uchumba,
mahusiano ya ndoa na nk. Sasa katika mahusiano ya ndoa wapo watu wengi
sana wanaruka hatua muhimu sana ambazo baadaye zinakuja kuwaumiza
vibaya. Hatua hizo muhimu ni urafiki na uchumba kwa hiyo, ikitokea watu
wamekutana ndani ya miezi miwili, mmoja na kukimbilia kufunga ndoa ndio
hawa wale wanaokuja kujuta kwa nini walifanya maamuzi hayo.
Mpendwa msomaji, malengo mahususi ya somo letu la leo ni madhara ya
kuchaguliwa mwenza katika maisha ya mahusiano. Ziko jamii tofauti
duniani zenye utaratibu au utamaduni wa kuwachanguliwa watoto wao wenza
pale wanapokua wamekaribia ule umri wa kuishi ya maisha ya ndoa kama mke
au mume. Wazazi wa jamii za kuwatafutia watoto wao wenza bado wapo
mpaka leo katika zama hizi za taarifa na pengine unafahamu watu ambao
wanafanya jambo hili kwenye jamii iliyokuzunguka.
Kwa mfano, mtoto tokea akiwa mdogo anawekewa ‘’ oda’’ mapema kuwa
wewe utaolewa na mtu fulani au utamuoa mtu bila kujali unataka au la.
Kwa hiyo, tabia hii inawanyima watoto wengi kuwa na mtu Yule anayempenda
badala yake wanakuwa na watu ambao siyo chaguo lao la kutoka moyoni.
Utamaduni huu unakuwa ni kama kumnyima mtu kuishi maisha anayotaka hapa
duniani.
Unaporuhusu wazazi wakuchagulie mwenza wa kuishi naye katika maisha ya ndoa kwanza inakuwa ni utumwa wa hali ya juu. Kwanini?
Kwa sababu kuchaguliwa kufanya kitu ambacho hukipendi katika maisha
yako ni utumwa. Vivyo hivyo, kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye ni utumwa
pia. Unapokuwa unachaguliwa mwenza wa kuishi naye unakuwa unavunja
hatua muhimu sana katika kuelekea maisha ya ndoa ambayo ni urafiki na
uchumba. Kupitia hatua hizi unaweza kumchunguza mwenzako ni mtu wa namna
gani, falsafa yake ya maisha ikoje, ni mtu chanya au hasi, ni mtu wa
kuigiza maisha au ni mtu halisi anayeishi bila kuigiza maisha na mambo
mengine mengi unayotaka kuyajua kutoka kwa mwenzako.
Rafiki, watu wanaoishi na wenza wao kwenye maisha ya ndoa kwa
kuchanguliwa na kwenda kuanza kuishi maisha ya urafiki, uchumba na ndoa
kwa wakati mmoja huwa wanashinda sana. unakuta mwenzako anaishi falsafa
tofauti kabisa na wewe ulivyotarajia. kwa mfano, wewe falsafa yako ni
kuishi chini ya kipato chako na unakuta mwenzako anataka kuishi juu ya
kipato kwa kufanya mambo ambayo hayana ulazima kwenye maisha. Lakini
kama ulikuwa umemgundua mwenzako na kumsoma vizuri katika hatua za
uchumba ungeweza kufanya maamuzi mapema kwa kumpima kama mtu huyo
anakufaa au la kulingana na vigezo vyako.
Kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye katika zama hizi ni aibu kwa kweli
kwani ni kuchaguliwa kufanya chochote ambacho hukipendi ni utumwa katika
maisha yako. Kumbuka rafiki, hata mzazi akikuchagulia mpenzi ambaye
wewe humpendi na ukakubali utakua umejichagulia wewe mwenyewe kuingia
shimoni. Kwa hiyo, hata wazazi wakikuchagulia kuishi na mwenza ambaye
wanampenda wao ni kama kuchaguliwa maisha ya kuishi hapa duniani. Licha
ya kuchaguliwa maisha wewe ndiye utakayeenda kuishi hayo maisha na wala
siyo wazazi watakaopata raha au shida, ukiingia shimoni wao hawatakuwepo
bali wewe ndio utawajibika.
Hatua ya kuchukua leo; usikubali kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye
katika maisha yako. Ishi na mtu unayempenda kutoka moyoni, ishi na mtu
ambaye mliweza kupitia hatua za urafiki, uchumba ukamjua vizuri tabia
zake ni mtu wa namna gani. Fanya kitu ambacho unakipenda ndio furaha ya
kweli katika maisha ambapo utapata mafanikio makubwa yenye furaha na
ubora wa hali ya juu.
Kwa kuhitimisha, tunaishi karni ya ishirini na moja na hatuko tena
katika zama za mawe bali tupo katika zama za taarifa. Kuwa chachu ya
mabadiliko kwa kuvunja utumwa huo katika jamii uliyopo siyo unasoma na
kupata elimu ya juu bado ukirudi nyumbani wazazi wanakushurutisha kuoa
au kuolewa na mtu Fulani bila ya ridhaa yako mwenyewe. Wewe ndio mwenye
maamuzi ya maisha yako kwa sababu hakuna mtu mwingine atakaye ishi
maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe.
COMMENT AND SHARE..................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!