Madaktari waonya kuhusu ulaji ''keki na peremende kazini'':;
on
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa kazini wakisema ugawanyaji wa keki na peremende unachangia matatizo ya kiafya.
Idara
ya afya ya meno imesema kuwa watu wanafaa kupunguza ulaji wa keki na
biskuti kazini kwa sababu vyakula hivyo vinawafanya kunenepa kupitia
kiasi mbali na afya mbaya ya mdomo.
Profesa Nigel Hunt amesema kuwa wafanyikazi wanahitaji kubadilisha utamaduni wa kazini.
Ili
kuweza kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari wafanyikazi
wameshauriwa kutumia vyakula hivyo kama chakula cha mchana mbali na
kuvificha .
Profesa Hunt ,muhadhiri wa chuo kikuu cha Royal
College of surgeons ,alisema kuwa huenda wasimamizi wa afisi hizo
wanataka kuwazawadi wafanyikazi, wafanyikazi kutaka kusherehekea ama mtu
anayeleta zawadi afisini baada ya likizo hatua inayosababisha vyakula
vya sukari nyingi kuingia afisini.
Lakini amesema kuwa hilo linaathiri afya ya wafanyikazi na ni muhimu
kufanya uamuzi wa mwaka mpya wa kukabiliana na utamaduni wa vyakula vya
sukari.
''Ijapokuwa peremende hizo huenda zikawa na maana
,zinachangia unenepaji wa kupitia kiasi pamoja na afya mbaya ya
mdomo,''aliongezea.
Tunahitaji kubadili utamaduni katika afisi
zetu ambao unashawishi ulaji wa vyakula vya afya na unawasaidia
wafanyikazi kutotumia vyakula vya sukari kama vile, keki, peremende na
biskuti.
COMMENT AND SHARE.....................!!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!