Mkoa wa Kagera umetakata katika matokeo ya mtihani wa upimaji wa kitaifa
wa darasa la nne kwa kukamata nafasi ya kwanza kitaifa licha ya mkoa
huo kukumbwa na janga la tetemeko la ardhi mwezi Septemba mwaka 2016.
Ufaulu
katika mkoa huo ni asilimia 98.83 ambapo jumla ya wanafunzi 48,334
wamefaulu kati ya wanafunzi 48,907 waliofanya mtihani, ikifuatiwa na
mikoa ya Kilimanjaro na Geita.
Katika matokeo ya mtihani huo
uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana (Miezi miwili baada ya tetemeko la
ardhi) Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba pia ambayo pia iko ndani ya
mkoa huo imeongoza katika halmashauri zote nchini.
Waliofaulu katika manispaa ya Bukoba ni
wanafunzi 2,927 kati ya wanafunzi 2,936, ufaulu ukiwa ni asilimia 99.69
ikifuatiwa na Mji Makambako, na Tanga Mjini kama inavyoonekana katika
majedwali yafuatayo.
Taarifa iliyotolewa leo na Baraza la
Mitihani la Taifa (NECTA) kupitia kwa Katibu Mtendaji wake, Dkt. Charles
Msonde, amesema jumla ya wanafunzi 950,167 kati ya wanafunzi 1,017,713
sawa na asilimia 93.36 waliofanya upimaji huo wameweza kupata alama
zenye madaraja ya ufaulu wa A, B, C na D.
Amesema wanafunzi 67,547 sawa na asilimia 6.64 wamepata alama za daraja la E lenye ufaulu usioridhisha.
Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa
wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Stadi za Kazi, Haiba Na
Michezo, ambapo asilimia 94.67 wamefaulu, huku wakifanya vibaya zaidi
katika somo la English Language lenye ufaulu wa asilimia 72.51.
Katika wanafunzi 10 bora kitaifa,
wanafunzi 8 ni wasichana wakiongozwa na Loi Martin Kitundu kutoka
Fountain Of Joy, huku wanafunzi wawili pekee wakiwa ni wavulana.
Baraza hilo pia limeyafuta matokeo ya wanafunzi 58 waliobainika kufanya udanganyifu.
COMMENT AND SHARE.................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!