JINSI YA KUPATA/KUZUIA SIMU ILIYOPOTEA AU KUIBIWA.
Hello! Habari.
Hivi karibuni mdau mmoja wa blog hii alinitumia e-mail na kuniuliza ni
kwa jinsi gani anaweza kuipata simu yake iliyopotea, hasa kwa kutumia
mtandao. Juhudi zangu za kutambua ni aina gani ya simu aliyoipoteza mdau
huyu bado hazijazaa matunda lakini ni matumaini yangu kuwa ataweza
kusoma post hii maalumu kwa ajili yake na wote wenye tatizo kama lake.
Hivi sasa tunapoongelea simu, tunaegemea sana kwenye smartphone.
Smartphone kwa kiasi kikubwa ni nyepesi kufanya shughuli nyingi ikiwemo
shughuli za usalama. Hivyo kwa kutumia uwezo wake huo tutaona jinsi ya
kuipata pindi inapopotea au inapoibwa. Lakini pia kama unatumia simu ya
kiganjani ya kawaida tutatizama pia jinsi ya kuipata.
Kama simu yako iliyopotea ni ya Apple ningependa ubofye hapa uendelee na Apple moja kwa moja.
Jinsi ya kupata simu iliyopotea: Android:
Simu hizo huwa moja wapo kati ya hizi:
TECNO,
SAMSUNG SONY, na nyingine nyingi za aina hizi.
Kama simu yako iliyopotea ni android usiwe na wasiwasi. Hebu tufuatilie
njia zifuatazo zinazoelezea kwa kina namna gani ya kuweza kuipata simu
yako.
>> Kwa kutumia ANDROID DEVICE MANAGER (ADM).
Je,
unatumia Google Play Store. Jibu lako bila shaka ni ndio na kama sio
basi hakikisha umejiunga na Play Store. Kwa nini nimeanza na hili ni kwa
sababu ili kujiunga na Play Store lazima uwe na akaunti ya Gmail. Kwa
nini Gmail, kwa sababu hii ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kutambua
pahala simu yako ilipo. Android Device Manager ni programu ya google
inayopatikana karibu katika kila smartphone ya android. Usijiulize
maswali mengi na hata kama haujawahi kuiona usiwaze, hii hufanya kazi
ndani ya smartphone yako. Jaribu kuisachi kama usipoipata unaweza
kidownload kupitia Play Store au
bofya hapa.
Programu hii itatusaidiaje?
ADM hufanya kazi ya kutambua pahala simu yako ilipo kwa wakati husika
endapo imeunganishwa na mtandao wa internet. ADM pia huweza kulock au
kufuta simu nzima kama umeifanyia settings. Kama simu yako imepotea au
imeibiwa fanya yafuatayo ili kuipata.
- Ni rahisi sana. Kama umetimiza yote hapo juu, punde tu unapogundua
simu yako imepotea tafuta laptop/computer au simu ya android nyingine
yoyote. Sign-in katika gmail kupitia kifaa hicho. Ukisha Sign-In
tembelea tovuti ya ADM hapa. Au search tu google 'Android Device Manager' na chagua tovuti yao pale juu kabisa.
- Tovuti hiyo ikishafunguka utaweza kuchagua kifaa chako (Smartphone/Tablet) ambayo imeshajisajili kupitia e-mail yako ya gmail.
- Baada ya kuchagua Google itakuonesha ramani ya wapi simu hiyo ilipo.
Baada ya hapo unaweza kuchagua kitufe cha ring. Hata kama aliyeiiba
ameshabadili line simu hiyo itaita kwa muda wa dakika kama tano.
- Zaidi pia ni jinsi ya kulock simu yako kupitia huduma hii hii ya
ADM. Utaweza kufanya hivyo kwa kuchagua kitufe cha Lock. Kumbuka kitufe
hiki kifanya kazi endapo ulifanya settings za kuruhusu ADM kulock na
kufuta simu. Faida moja wapo pia ya kutumia option hii ya Lock ni kwamba
unaweza kuandika ujumbe ambao yeyote mwenye simu hiyo kwa wakati huo
ataiona.
- Pia unaweza kufuta data zote zilizopo katika simu yako hiyo kama
unahisi imeibwa au imepotea kabisa kwa kubonyeza kitufe cha Erase.
Njia hii huweza kufanya kazi endapo tu, umeshajiunga na gmail, na pia
simu iwe imeunganishwa na internet. Hii ndiyo njia bora kwa mujibu
wangu. Usipofanikiwa mara ya kwanza endelea kujaribu usikate tamaa, kama
mwizi ameiba smartphone lazima nyakati fulani ataingia tu katika
mtandao. Akiingia tu basi kajichanganya. Ni vyema utoe taarifa polisi ni
wajibu wao kuhakikisha usalama wako na mali zako.
Plan B ni
app ambayo imetengenezwa kama suluhisho wa ADM. Plan B inakuwezesha
kutambua mahali simu yako ilipo kwa kuinstall programu kupitia mtandao.
Hii inakusaidia kama mwanzo haukuwa na ADM na kwa sababu imepotea hauna
uwezo wa kudownload na kuinstall. Plan B itakutumia SMS kila baada ya
dakika 10 kukupa taarifa juu ya simu yako na mahali ilipo.
Njia nyingine ni pamoja na kutumia apps ambazo itabidi uzi install kabla ya kuibiwa (:))
Apps hizo ni kama hizi zifuatazo:
Unaweza kutumia
Google Maps pia kufuatilia mwenendo wa simu yako. Kama una akaunti ya Gmail utakuwa tayari umeunganishwa na Google Maps. Tembelea
Google Maps kisha nenda katika
Settings chagua
Location History. Kwa njia hii utaweza kugundua mahali simu yako ilipo.
Je kama simu yangu sio smart kivile?
Kama simu yako ni simu tu ya kawaida ya mawasiliano kama Nokia ya tochi,
inapoibiwa au kupotea siyo rahisi kuitafuta kwa njia ya mtandao. Kama
unaifahamu IMEI namba, ambayo ni tofauti kwa kila simu unaweza
kuiunganisha simu yako hapa katika mtandao wa TrackImei na itaweza
kutafuta mahala simu hiyo ilipo pindi itakapo potea.
Asante kwa kusoma hii. Shukrani kwa kuwa nasi mwaka mzima wa 2014.
Mipango yetu kwa ajili yako ni mikubwa zaidi 2015. Endelea kuwa nasi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!