Klabu ya Manchester City imepata
idhini ya kumnunua rasmi winga wa Brazil wa umri wa miaka 19 Gabriel
Jesus na sasa anaweza akacheza dhidi ya Tottenham Jumamosi.
Jesus amehamia City kutoka klabu ya Palmeiras ya Brazil kwa £27m.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikubali kuhamia City kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana.
Alisalia na Palmeiras hadi mwisho wa msimu wa soka Brazill mwezi Desemba.
"Ana uwezo wa kuibuka kuwa miongoni mwa washambuliaji bora zaidi
katika soka," mkurugenzi wa soka wa City Txiki Begiristain alisema.
Jesus
alifika City mwanzoni mwa mwezi huu lakini alichelewa kupata idhini ya
kusajili wa City, taarifa zikisema Shirikisho la Soka la Uingereza
lilikuwa linachunguza stakabadhi kuhusu uhamisho wake.
City wanamchukulia mchezaji huyo kuwa chipukizi mwenye kipaji zaidi Amerika Kusini kwa sasa, na waliwapiku Barcelona kumchukua.
Jesus amesema meneja wa City Pep Guardiola alichangia sana katika uamuzi wake wa kuhamia klabu hiyo.
City
kwa sasa wamo nambari tano kwenye jedwali Ligi ya Premia, alama 10
nyuma ya viongozi Chelsea baada ya kulazwa mechi mbili kati ya tatu
walizocheza karibuni zaidi.
Mbona anaitwa Jesus?
Jesus alikuwa awali akifahamika kama Gabriel Fernando alipoanza kuchezea kikosi cha kwanza Palmeiras akiwa na miaka 17.
Taarifa
ya City imesema: "Akifahamika wakati huo kama Gabriel Fernando, alipewa
jezi nambari 33 - umri wa Kristo - na afisa mmoja wa habari wa
Palmeiras alimshawishi kubadili jina na kuwa Gabriel Jesus.
"Alichezeshwa
katika timu kuu ya Palmeiras mara ya kwanza na Oswaldo de Oliveira
mnamo 7 Machi 2015, alipoingia dakika ya 73 mechi ambayo walishinda 1-0
dhidi ya CA Bragantino katika uwanja wa Allianz Parque."
COMMENT AND SHARE........................!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!