Takwimu
zilizotolewa na idara ya Marekani ya Kilimo (USDA) zimeonyesha
kwamba nchi zilizoendelea zina asilimia ndogo ya matumizi ambayo
hutumika kwa ajili ya chakula kwenye familia ukilinganisha na nchi
ambazo zinazoendelea.
Takwimu
hizo zimeeleza kuwa katika nchi ambazo zinatumia zaidi kipato cha
familia kwa ajili ya chakula ni pamoja na Nigeria ambayo imetajwa
kutumia zaidi ya nusu ya kipato cha familia kwa ajili ya chakula ambapo
pia kuna nchi zaidi ya tisa ambazo zimetajwa kutumia zaidi ya 40% ya
kipato cha familia kwa ajili ya chakula.
Kwa
Afrika zipo nchi nne kwenye hiyo list ambapo ni Nigeria 56.4%, Kenya
46.7%, Cameroon 45.6%, na Algeria 42.5% lakini nje ya Afrika ni
Kazakhstan 43.0%, Philippines 41.9%, Pakistan 40.9%, Azerbaijan 40.1%.
Guatemala 40.6%.
Takwimu
hizo zimeeleza kuwa kuna nchi nane ambazo hutumia chini ya 10% pato la
familia kwa ajili ya chakula, nne zipo Ulaya ambazo n i pamoja na
Uingereza ambayo ni ya tatu ikiwa na 8.2% ikifuatiwa na Uswisi
kwa 8.7%, Ireland 9.6% na Austria 9.9%.
Mataifa mengine ni Marekani ambayo inatumia 6.45%, Singapore ni ya pili ikiwa na 6.7%, Canada ni 9.1 wakati Austria 9.8%.
COMMENT AND SHARE..................!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!