Mwanamuziki wa bongofleva nchini Tanzania anayefanya vizuri na wimbo
wake wa Muziki, Darassa kwa mara ya kwanza amekiri kuwa aliwahi kwenda
kwa mganga wa kienyeji ili amsaidie atoke kimaisha.
Darassa aliyasema hayo jana usiku alipokuwa katika kipindi za Ala za
Roho cha Clouds Fm ambapo mtangazaji alitaka kujua kama aliwahi kwenda
kwa mganga tangu azaliwe.
Nimewahi kwenda kwa mganga mara moja, ni kipindi cha nyuma kidogo.
Nilikwenda kwa mganga baada ya maisha kuwa magumu sana nikiamini ataweza
kunisaidia. Unajua mimi nimekulia uswahilini na kule ukiwa kijana
kunakuwa na mambo mengi sana, hivyo nilishawishiwa nikakuta nimeenda,
alisema Darassa.
Darassa alisema baada ya kufika kwa mganga aliona kuwa mganga hawezi
kumsaidia na tangu alipoondoka hakurudi tena. Aidha, alisema kuwa
aliacha kuamini kwenye masuala ya kishirikina kwani ndio kikwazo kikubwa
cha wakazi wengi wanaoishi uswahilini hawaendelei.
Darassa amewaasa watu mbalimbali wanaoamini katika imani za kishirikina
kuwa hazitawasaidia na badala yake Mungu yupo na wakimuamini atawasaidia
kama ambavyo imekuwa kwake ambapo ametoka kwenye maisha ya dhiki sana.
Alipoulizwa kama ajali yake iliyotokea mwezi uliopita aliuhususha na
kulogwa, alisema kuwa yeye hakuihusisha na imani za kishirikina na kuwa
sababu kubwa ya ajali ni uchovu tu licha ya baadhi ya watu kusema kuwa
na mambo ya kishirikina.
COMMENT AND SHARE......................!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!