WATU
saba, akiwamo mmoja anayedaiwa kuwa daktari bandia, wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kutengeneza
kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano na kuziuza kwa watu wanaofika
hospitali ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Chanjo hizo ni zile ambazo hutolewa kwa watu ambao wanasafiri nje ya nchi kama kinga kwa ajili ya homa manjano.
Kamishna
wa Kanda hiyo, Simon Sirro, akizungumza jana na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, alimtaja aliyejifanya daktari kuwa ni
mfanyabiashara Salum Natali (47), mkazi wa Chanika Magengeni.
Kamanda
Sirro aliwataja watuhumiwa wengine ni walinzi watatu ambao ni Aisha
Hassan (29) mkazi wa Vingunguti Mikoroshini, Yakobo Msenga (42) mkazi wa
Chanika na Junith Dunstan (23) mkazi wa Kiwalani.
Wengine
ni Oliver Bwegege (58) mkazi wa Kigogo Mkwajuni, mjasiriamali Fredy
Nyomeye (44) mkazi wa Chang’ombe na fundi umeme Mohamed Bwanga (59)
mkazi wa Majohe Gongo la Mboto.
Alisema
watu hao walikamatwa Januari 16, mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi
baada ya mtoa taarifa (jina linahifadhiwa) kufika hospitalini hapo na
kutakiwa kutoa fedha na mmoja wa watuhumiwa hao ili kupatiwa kadi hiyo
ya chanjo ya homa ya manjano.
“Katika
mahojiano, watuhumiwa hao walikiri kufanya kosa hilo la kughushi na
kutoa kadi hizo za chanjo pasi na mtu kuchomwa sindano yenyewe ya
chanjo,” alisema.
Kamishna Sirro alisema Natali alikuwa akijifanya kuwa ni daktari aliyekuwa akiwachoma watu sindano.
Alisema
uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kuwabaini washiriki wengine
katika mtandao huo wa utoaji wa kadi hizo bandia za chanjo bila kutoa
chanjo yenyewe husika.
Katika tukio
lingine, watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa na polisi baada
ya kudaiwa kuhusika kwenye tukio la mauaji Boko Basihaya, jijini Dar es
Salaam.
Sirro alisema inadaiwa kuwa watu
hao walihusika kwenye kifo cha mlinzi wa duka la pombe (Grocery)
aliyetajwa kwa jina la Marwa. Alisema watu hao wanadaiwa kumpiga risasi
kichwani mtu huyo na kupora Sh. milioni 1.3.
“Baada
ya tukio hilo Jumatatu ya wiki hii polisi walimkamata mwendesha
bodaboda, Nathan Mathias akiwa kwenye baa iitwayo PK eneo la Kawe,
ambaye alikiri kuhusika na tukio hilo na alimtaja Hamis Daudi mkazi wa
Boko njia panda Magereza kushirikiana naye.
“Polisi
walifanya upekuzi nyumbani kwa Daudi na kuipata silaha aina ya Shotgun
Pump Action yenye namba P. 918884 na TZCAR 76475 ikiwa na risasi mbili,”
alisema.
Alisema watuhumiwa hao
waliwaeleza polisi kuwa bunduki nyingine wameificha maeneo ya Ununio
kwenye mabwawa ya chumvi kando ya Bahari ya Hindi hivyo askari
walikwenda nao huko kwa ajili ya kuzichukua.
COMMENT AND SHARE.........................!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!