STORI: GABRIEL NG’OSHA, GAZETI LA UWAZI, TOLEO 1021, JANUARI 3-9, 2017
DAR ES SALAAM: Habari ya motomoto inaeleza kuwa Januari 16, mwaka huu
ndiyo siku ambayo mtoto wa kiume wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ atatimiza siku 40 tangu
alipozaliwa Desemba 6, mwaka jana.
Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa ndani ya familia ya
Diamond zilieleza kuwa, Nillan ambaye ni mdogo wa mtoto wa kwanza wa
staa huyo, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ anatarajiwa kufanyiwa
shughuli hiyo kubwa ya kumtoa ambayo itafanyika nyumbani kwa jamaa huyo
huko Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Taarifa nyeti zilieleza kuwa, tayari baadhi ya watu wao wa karibu Bongo
wamefikishiwa kadi ambapo watakwenda Sauz na kurudi kwa usafiri maalum
wa ndege ambapo kila kitu watakuwa wameshalipiwa.
“Tayari Diamond ametoa kadi maalum kwa watu wake wa karibu. Waliopewa
kadi wanatakiwa kuthibitisha kama watahudhuria ili kuweka mambo sawa na
kujua idadi kamili ya watakaokwenda kwa ajili ya kuwagharamia.
Mtoto wa kwanza wa Diamond, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ akiwa kalala na Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’ .
“Unaambiwa siku hiyo (Januari 16), watu watakula bata la kufa mtu maana shughuli ya Chibu Junior itaifunika ile ya Tiffah.
“Mbali na mastaa na watu wa kila aina kualikwa kutoka Bongo lakini pia
40 ya Chibu Junior itahudhuriwa na mastaa wakubwa Afrika ambao wengi ni
rafiki zake Diamond hasa wa kutoka Nigeria,” kilifunguka chanzo chetu
kikiomba chondechonde kisitajwe popote.
Mbali na chanzo hicho, mtu mwingine ndani ya familia hiyo alipoulizwa
juu ya taarifa za mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kuhamia Sauz kwa
ajili ya shughuli hiyo alisema kuwa, si kwamba tu amehamia lakini kwa
sasa mzaa chema huyo ameshakuwa mwenyeji wa mitaa ya Johannesburg
kufuatia kuwa huko tangu alipojifungua mkwewe, Zarinah Hassan ‘Zari The
Boss Lady’, Desemba 16, mwaka jana.
Hata hivyo, alipotafutwa Diamond hakuwa hewani ambapo mmoja wa
wanafamilia alisema kuwa yupo nyumbani kwake Sauz kwa mapumziko ya
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa 2017.
“Jamaa hayupo Bongo labda umcheki kwa WhatsApp, yupo Sauz home kwake si
unajua mambo ya bata za sikukuu ya mwaka mpya? Kwani kuna ishu gani?,”
alihoji mwanafamilia huyo kwa sharti la kutotajwa kwani siyo msemaji wa
familia ya Diamond.
Alipoulizwa juu ya 40 ya mdogo wa Tiffah na kwamba kuna mwaliko maalum na itakuwa bab’kubwa, jamaa huyo alifunguka:
“Ebana hiyo shughuli achana nayo kabisa lakini unachotakiwa kujua ni kwamba itampaisha Chibu Junior Afrika nzima.”
COMMENT AND SHARE.........................!!!!!!!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!