Simu za
Smartphones zimekuwa ni kati ya vitu vinakimbizana na teknolijia kila
kukicha, na ni moja kati ya vifaa ambavyo vimekuwa seheme ya maisha ya
karibu asilimia 70 ya watu duniani lote, kuna wakati simu tunazomiliki
zimekuwa zinatoa majibu ya wewe ni mtu wa aina gani.
Simu zimekuwa zikitengenezwa kuleta ushindani wa teknolojia lakini kupima uwezo wa kifedha wa watumiaji na mapenzi.
Kwa mujibu
wa The Merkle wamezitaja aina 5 za simu ambazo mpaka kufikia mwezi
December 2016 zimekuwa ni simu zilizovunja rekodi ya kuuzwa kwa bei ya
juu kuliko simu nyingine zozote duniani. Japokuwa hizi simu ni za
kawaida ila tu zimekuwa zikiongezewa urembo wa madini ya thamani kubwa
ili kuzipa muonekano wa kipekee .
5.- GOLDVISH LE MILLION ($1.3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 2.8)
Sifa ya
hii simu ukiishika kama sio mmliki wake inapiga kelele zenye sauti ya
kuonesha imeibiwa. Cover la nje lote limeunda kwa Almasi ya
Karat 120, na cover la ndani limeundwa kwa dhahabu ya kutosha.
4.- DIAMOND CRYPTO SMARTPHONE ($1.3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 2.8)
Simu hii
imeundwa na mtaalmu wa madini aitwaye Peter Aloisson na ilitoka kwa mara
ya kwanza mwaka 2006, Simu hii ya Diamond Crypto Smartphone iliundwa
kwasababu maalumu za kutunza siri, kwa mujibu wa watengenezaji wake.
Simu hii hutumia OS ya Windows CE kama mfumo mkuu wa uendeshaji wake.
Simu hii imeundwa kwa madini ya Almasi ambapo kuna vipande 50 pia vya
Almasi ya blue.
3.- AMOSU CALL OF DIAMOND IPHONE 6 ($3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 6.5)
Alexander
Amosu ndiye mtengenezaji wa simu hii ambaye mwanzo alikuwa akifanya
baishara ya kuuza ringtone za simu. Kwasasa anaziongezea urembo simu na
kuziuza kwa mastaa wa muziki, wacheza filamu, wanamichezo pamoja na watu
maarufu wenye uwezo mkubwa kifedha.
The Call
of Diamond ni simu aina ya iPhone 6 ambayo imenakshiwa kwa Gold ya Karat
18 kwenye cover lake la ndani wakati kwa nje imewekewa vipande vya
Almasi vinavyofikia 6,127 na inamaliziwa na logo ya Cupertino moja ya
makampuni makubwa duniani.
2.- BLACK DIAMOND IPHONE 5 ($15 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 32.6)
Kama
ulidhani dola milioni 3 ni nyingi kununua simu sasa kutana na hii,
inaitwa Black Diamond iPhone 5. Simua hii imeundwa kwa Gold inayifikia
Karat 26, Almasi iliyotiwa rangi nyeusi pia imeongeza urembo kwenye simu
hii. Black Diamond inatengenezwa na kampuni ya mfanyabiashara kutoka
China anaitwa Stuart Hughes.
1.- FALCON SUPERNOVA IPHONE 6 ($100 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 217.8) Bila shaka umeona gap lililopo kutoka simu
iliyoshika nafasi ya pili! Hii ni iPhone 6s ambayo kila kitu kilichopo
kwenye simu hii ni madini ya Almasi, Gold pamoja na Ruby. Mzigo unaitwa
The SuperNova pamoja na bei hiyo bado unaambiwa hii sio simu ya gharama
kati ya zilizowahi kuundwa.
COMMENT AND SHARE........................................!!!!
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!