Umoja wa Mataifa umezihimiza kuwepo
kwa utulivu nchini Gabon baada ya fujo kuzuka kuhusiana na utata kuhusu
matokeo ya uchaguzi wa urais.
Baraza la Usalama la umoja huo
limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake kujizuia kufanya
uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za kisheria.
Maafisa wa usalama kufikia sasa wamewakamata watu zaidi ya elfu moja baada ya siku ya pili ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.
Upinzani unadai Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.
Watu watatu waliuawa mji mkuu Libreville.
Rais Omar Ali Bongo na kiongozi wa upinzani Jean Ping
Rais Bongo amesisitiza kwamba alishinda kwa njia halali na kuutaja ushindi wake kuwa ushindi wa watu wa Gabon.
Amesema kuna kundi ndogo la watu wachache waliotaka kutwaa madaraka na ambao wameshindwa.
Matokeo
ya uchaguzi yalitangazwa Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi
kwa 49.8% ya kura, akifuatwa na Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura
zilizowatenganisha zikiwa 5,594.
Bw Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na "hakuna ajuaye" hasa nani alishinda.
Upande wa Bw Ping unasema takwimu kutoka ngome za rais huyo
zinaonyesha asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza. Ameomba takwimu za
wapiga kura kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Bw Bongo aliingia madarakani mwaka wa 2009, baada ya kifo cha babake aliyekuwa ameongoza taifa hilo tangu 1967.
Kabla ya kuingia katika siasa, Ping aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
COMMENT AND SHARE...................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!