ELIZABETH Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa
kortini jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za
kuandika maneno ya kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa
kijamii wa What’s App.
Akisomewa mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya
Hakimu Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho
kilicho kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.
Wakili Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa
huyo aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;
“….Rais kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli…
f****l** lile, kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na
ukiamka asubuhi ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi
mwanzo mwisho.”
Hata hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa
serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Mtuhumiwa alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili
huku kila mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.
Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.
COMMENT AND SHARE........................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!