MWANAFUNZI aliyekuwa akisoma Darasa la Saba katika Shule ya Msingi
Zimba, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga, Susana Kauzeni (15)
ameuawa baada ya kupigwa na
wazazi wake wakimtuhumu kuwa ni mtoro sugu wa shule.
Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Shule za Msingi),
Peter Fusi amesema kuwa mwanafunzi huyo alizikwa kijijini humo Julai
23, mwaka huu.
“Baba na mama yake walichangia kumpiga binti yao huyo wakimtuhumu
kuwa ni mtoro sugu wa shule pia nyumbani amekuwa haonekani. Baba yake
mzazi amekimbia baada ya kufanya uhalifu huo huku mama yake akiwa
ameshikiliwa na Jeshi la Polisi,” alieleza Fusi.
Fusi alieleza kuwa kuanzia Agosti 3 na 4, mwaka huu alitembelea
baadhi ya shule za msingi zilizopo kwenye Bonde la Ziwa Rukwa ikiwemo
Shule ya Msingi Zimba kufuatilia kazi ya utengenezaji wa madawati mapya
kwa ajili ya shule za msingi pia kufuatilia takwimu sahihi za wanafunzi
ili kubaini wanafunzi hewa.
“Nilipofika kwenye Shule ya msingi Zimba, Mratibu Elimu Kata, Daudi
Moga na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Fidelis Mwangurumba walithibitisha
kutokea kwa mauaji hayo ya mwanafunzi huyo,” alisema.
Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwangurumba, mwanafunzi
huyo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi watoro sugu shuleni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!