Vikosi mbalimbali vya majeshi ya ulinzi na usalama katika manispaa ya
BUKOBA mkoani KAGERA hii leo vimefanya mazoezi ya wazi ya utayari na
utimamu
Vikosi mbalimbali vya majeshi ya ulinzi na usalama katika manispaa ya
BUKOBA mkoani KAGERA hii leo vimefanya mazoezi ya wazi ya utayari na
utimamu wa mwili hali iliyosababisha hofu kwa baadhi ya wakazi wa eneo
hilo.
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Mkuu wa mkoa wa KAGERA meja
jenerali mstaafu SALUM KIJUU ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya mkoa, amewatoa hafu wananchi na kusema lengo la
mazoezi hayo ni kujenga mahusiano mazuri miongoni mwao na jamii
inayowazunguka.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa KAGERA meja jenerali Mstaafu SALUM
KIJUU amesema mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika mara mbili kwa kila
mwezi hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na shaka yoyote.
COMMENT AND SHARE.................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!