Vidonda vya Tumbo: Ni nini na husababishwa na nini haswa?:;
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na
umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na
mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio
'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo
mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru
'Rectum'.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo
mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika
kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii
hutambulika kama 'Peptic ulcers'.
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita
vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita
'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'
VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda
vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs
husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana
kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati
mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza
vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi
kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza
maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu
madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa
hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa
na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics'. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya
tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu
kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress'. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda
moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Hata hivyo ni mara chache sana mtu kuugua vidonda vya tumbo na kutoonyesha dalili.
Zifuatazo ni dalili zinazotokea kwa wagojwa wengi:-
=> Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali
wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula
chakula kidogo.
=> Kushindwa kumeza vizuri chakula.
=> Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
=> Kujisikia vibaya baada ya kula.
=> Kupungua uzito.
=> Kukosa hamu ya kula.
DALILI HATARI
=> Kutapika damu.
=> Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
=> Kichefuchefu & kutapika.
JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-
Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteka wake ni vidonda vya tumbo.
Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-
=>Kupima damu 'Blood test'. Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na
kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton
Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu
vitaonyesha majibu hasi 'Negative'
=>Kupima pumzi 'Breath test'. Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi
za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika
na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama
mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni
kwenye kabonidioksaidi.
=>Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'. Kipimo hiki
huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi. Vilevule kipimo
hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya
bakteria.
=>X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'.
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum.
Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana
kirahisi kwa x-ray.
Kamera ya tumbo 'Endoscopy'. Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni
na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.
Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana
maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump
Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole, Esomeprazole & Lansoprazole.
Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya
protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa
asidi tumboni.
Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatalithiwa na dawa kama Paracetamol.
Vilevile dawa aina ya H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine, hutumika kama mbadala kama dawa aina ya 'PPIs' hazitokuwepo.
H2-Receptor Antagonists hufanya kazi ya kuzuiia utendaji wa protini
iitwayo 'Histamine' ambayo inahusika na kuchochea utengenezaji wa asidi
tumboni.
Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya
kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama
vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya
haraka.
Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!