Uturuki:Kundi la IS linapaswa kutokomezwa kabisa:;
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki
Mevlut Cavusoglu amesema kundi la Islamic state linatakiwa kuondolewa
kabisa kutoka mikoa ya kaskazini mwa Syria.
Amri hiyo inakuja huku
kukiwa na taarifa kwamba majeshi ya Uturuki yanajiandaa kushikilia mji
wa mpakani wa Jarablus ambao upo mikononi mwa I-S .
''Tutapigana
kuipinga Islamic State na taasisi nyingine za kigaidi mpaka mwisho.
Tutaendelea kuunga mkono nchi zote zinazopambana na vikundi hivyo. Kama
unavyojua wapiganaji wa upinzani wamefanikiwa kutekeleza mashambulizi
kadhaa AL-Rai na mpakani kwetu.
Kwa hakika, mikoa iliyo mipakani
lazima iwaondoe kabisa wapiganaji wa IS. Kwa kipindi hiki tutaendelea
kutoa ushirikiano ili kuwaondoa wapiganaji wa IS kutoka katika maeneo''
Wanamgambo
wa Islamic state wanashutumiwa kutelekeza shambulizi la bomu la kujitoa
mhanga lililotokea mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa Gaziantep
uliopo kusini mwa Uturuki.
Shambulizi hilo lililenga harusi iliyokuwa ikiendelea ambapo takribani watu hamsini waliuawa ,wengi wao wakiwa ni watoto.
Uturuki imeshambuliwa mara kadhaa mwaka huu huku shambulizi la juma lililopita likitajwa kuwa baya zaidi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!