Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WEST), kwa mujibu wa Waraka
Namba 4 wa mwaka 2014, imeipa Taasisi ya Elimu Tanzania mamlaka ya
kufanya uthibiti wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia. Itakumbukwa kuwa kabla ya mwaka 2014, ithibati kwa vitabu na
vifaa vya kielimu ilikuwa inatolewa na Kamati ya Ithibati ya Vitabu na
Vifaa vya Kielimu (EMAC), ambayo ilivunjwa mwaka 2013.
Kwa
muktadha huo, Wizara inawaagiza wachapishaji wote wa vitabu vya Darasa
la Nne hadi Darasa la Saba ambavyo vina ithibati ya EMAC kuviwasilisha
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini. Ili
kufanikisha zoezi hili nakala nne (4) za kila chapisho ziwasilishwe kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya tarehe 30
septemba, 2016. Baada ya muda huo kupita, vitabu vyote ambavyo
havitakuwa vimewasilishwa na kuhakikiwa na Taasisi hiyo vitafutwa katika
orodha ya vitabu vyenye ithibati.
Baada ya zoezi la uhakiki
kukamilika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na OR
– TAMISEMI, itafanya ufuatiliaji kwenye shule na maduka ya vitabu ili
kuhakiki utekelezaji wa agizo hili.
Aidha, hatua stahiki zitachukuliwa kwa wauzaji/wachapishaji watakaoendelea kuuza vitabu vitakavyokuwa vimefutwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!