Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22
Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza
kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4
Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni
tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.
Waombaji wapya na baadhi ya waombaji
walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3
Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia
Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji
wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.
Baraza linapenda pia kuwaarifu
waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha
majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS)
vilipitisha orodha ya majina ya wenye sifa za udahili kulingana na
nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe
18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa
kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa
Udahili wa Pamoja (CAS). Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa
kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.
Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE
na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili
kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama
Serikali ilivyoagiza.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Tarehe: 22 Julai, 2016
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!